Preloader logo
Menu

Ulinzi zaidi, Haraka,
Ufikiriaji wa mbele.

DigiByte ni haraka zaidi ya sarafu ya kidigitali. Ni blockchain ya uvumbuzi kwa ajili ya mali za kigitaili, smart contracts, programu zenye madaraka na uthibitisho salama.

Mwongozo wa ujumuishaji

Kipi kinaifanya DigiByte kuwa na nguvu zaidi ya wengine?

DigiByte ni chanzo -wazi cha blockchain kinachokua kwa haraka kilichoundwa mwishoni mwa mwaka 2013 na kutolewa mapema mwaka 2014. Baada ya miaka ya maendeleo ya ufikiriaji wa mbele, DigiByte imekuwa moja ya blockchain yenye usalama, kasi, ndefu na UTXO blockchain yenye madaraka.

Isiyohodhiwa kabisa

DigiByte haijawahi kufadhiliwa kupitia ICO au kiwango muhimu cha sarafu zilizochimbuliwa awali. Hakuna Mkurugenzi Mtendaji au kampuni inayodhibiti blockchain ya DigiByte. Ni mradi wa kujitolea unaendeshwa kijamii.

Salama zaidi.

DigiByte hutumia algorithms 5 za kimfumo na marekebisho ya ugumu wa wakati halisi ili kuzuia ujumuishaji mbaya wa uchimbaji na kushuka kwa hash power. Mojawapo ni Odocrypt inayojibadilisha yenyewe kila baada ya siku 10 kwa ukinzani wa ASIC.

Haraka zaidi.

DigiByte blocks zinatokea kila baada ya sekunde 15 ambayo ni mara 40 haraka zaidi ya Bitcoin na mara 10 haraka zaidi ya Litecoin. Utekelezaji wa mapema wa SegWit na ugumu wa blockchain unawezesha mpaka miamala 1066 kwenye mnyororo Kwa sekunde kwa ada ambazo ni ndogo sana.

Ufikiriaji wa mbele.

Kwa zaidi ya miaka sasa, DigiByte imekuwa ikijirudia yenyewe mbali na blockchain nyingi kama DigiShield, MultiAlgo, utekelezaji wa SegWit, Odocrypt algorithm, Dandelion++ privacy protocol, DigiAssets na Digi-ID.

Nini maana ya DigiByte? Angalia video ya utangulizi

Hivi ndivyo blockchain ya DigiByte inavyofanya kazi.

Safu tatu ndizo sehemu kuu za uvumbuzi kwenye blockchain ya DigiByte zinazotoa miundombinu ya mtandao, ulinzi na mawasiliano katika ufanyaji kazi wa spidi ya ajabu.

Programu / DigiAssets.

Safu ya juu ni kama stoo ya programu iliyo na mwonekano na matumizi halisi ya dunia. Aina zote za mali za kigitail zinaweza kuundwa kupitia itikadi ya DigiAssets juu ya blockchain ya DigiByte. Programu zilizo na madaraka (dApps) zinaweza kuundwa juu ya blockchain ya DigiByte. Pia smart contracts zilizo ngumu na salama juu blockchain ya DigiByte zinaweza kuundwa kwa urahisi.

Mali za kigitaili / Kitabu cha umma.

Safu/Tabaka la katikati hutoa usalama/ulinzi na utawala. Digital Byte ya data, huwakilisha data nyingi au kizio kinachoshikilia thamani na haiwezi kuwa bandia, kurudiwa au kufanyiwa utapeli. Kitabu/daftali la umma lenye ulinzi wa hali ya juu ambapo shughuli/miamala yote ya DigiByte inatunzwa. DigiByte inatumia algorithm tano kuthibitisha kazi kwa ajili ya ulinzi. DigiByte mpya hutokana na uchimbaji pekee.

Kiini cha itifaki / Mtandao wa ulimwengu.

Safu/Tabaka la chini hutoa mawasiliano na taratibu za ufanyaji kazi. Ni kiwango cha chini kabisa cha node kwenye DigiByte cha mawasiliano katika mtandao wa ulimwengu. Maelfu ya watu wanatumia programu ya DigiByte kote ulimwenguni. Seva, kompyuta, tablet au simu yoyote iliyounganishwa na mtandao wa DigiByte inakuwa node inayosaidia kupokea na kuruhusu miamala/shughuli. Anza kuchangia kwenye blockchain ya DigiByte kwa njia bora.

Chanzo-wazi / Kisichohitaji ruhusa.

Kama ilivyo tovuti, DigiByte blockchain ni chanzo-wazi na kisicho na gharama kutumia kilichotolewa chini ya leseni ya MIT, ambacho kinakupa nguvu ya kuendesha na kubadilisha programu. Uwazi unaruhusu uthibitisho huru wa binary na chanzo cha misimbo/code zinazoendana.
Itifaki ya DigiByte kwenye GitHub.
Kiini cha maendeleo ya DigiByte kwenye GitHub.

Stigi za DigiByte blockchain

Historia ya DigiByte.

Vumbua hatua muhimu za maendeleo makubwa ya blockchain ya DigiByte.

Development

Maendeleo ya muda wote yameanza ili kujenga blockchain ya DigiByte ya siku za usoni.

Oktoba, 2013 Jifunze zaidi
Launch

Block ya mwanzo ilichimbwa kwa ukamilifu na blockchain ya DigiByte kuzinduliwa rasmi.

Januari 10, 2014 Jifunze zaidi
DigiShield

GigiShield iliwezeshwa kutumia mabadiliko ya muda kamili dhidi ya kupanda na kushuka kwa hash.

Februari 28, 2014 Jifunze zaidi
MultiAlgo

MultiAlgo iliwezeshwa kutumia algorithms 5 tofauti ili kuzuia kuhodhiwa kwa madaraka ya Uchimbaji.

Septemba 1, 2014 Jifunze zaidi
MultiShield

MultiShield iliwezeshwa kupanua ulinzi wa DigiShield zaidi ya algorithm 5 za uchimbaji.

Desemba 10, 2014 Jifunze zaidi
DigiSpeed

MultiSpeed iliwezeshwa kupunguza muda wa block mpaka sekunde 15 kwa kufanya miamala haraka.

Desemba 4, 2015 Jifunze zaidi
SegWit

SegWit iliwezeshwa kabla ya Bitcoin na Litecoin kwa ajili ya matumizi ya ukubwa wa block.

April 28, 2017 Jifunze zaidi
Digi-ID

Digi-ID ilizinduliwa kuwezesha watumiaji kuweka jitihada kidogo kuingia kwenye tovuti na zaidi.

Mei, 2018 Jifunze zaidi
DigiAssets

DigiAssets ilizinduliwa kuwezesha utoaji madaraka ya mali na zaidi.

Aprili, 2019 Jifunze zaidi
Dandelion++

Protakali ya Dandelion++ ilianzishwa kuzuia ufuatiliaji IP na eneo.

Mei 3, 2019 Jifunze zaidi
Odocrypt

Odocrypt iliwezeshwa ambayo inabadilika yenyewe kila baada ya siku 10 Kwa ajili ya ukinzani wa ASIC wenye nguvu.

Julai 21, 2019 Jifunze zaidi
Roadmap
Ili kujifunza zaidi kuhusu mabadiliko yanayopendekezwa kwa itifaki ya DigiByte, tafadhali tembelea hifadhi ya DIPs: Hifadhi ya DIPs ya DigiByte
Ili kujifunza zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kuchangia maendeleo ya DigiByte, tafadhali tembelea jukwaa la Majadiliano la GitHub: Majadiliano ya GitHub ya DigiByte

Sarafu ya kidigitali ambayo
utaipenda kwa ujumla.

DigiByte (DGB) ni sarafu ya kidigitali ambayo inaweza kupanuka kutoka hatua moja kwenda nyingine na inawezesha kasi kubwa ya ufanyaji miamala kwa ada ndogo sana. DigiByte ni njia nzuri ya kufanya malipo.

Jifunze kwa kutazama

Rahisi kutumia.

Kuanza kutumia DigiByte ni rahisi zaidi kuliko hata kutuma meseji. Unaweza kutuma na kupokea DigiByte kwa kutumia vifaa ambavyo tayari unavijua na kuvipenda. Unachotakiwa ni kuweka Pochi inayopokea DigiByte kwenye kifaa chako alafu bonyeza scan, scan QR code na tuma DigiByte. Rahisi kama 1..2..3.

Sio ICO.

DigiByte haijawahi kufadhiliwa kupitia ICO au kiwango muhimu cha sarafu zilizochimbuliwa awali (0% iliyobaki). Hakuna Mkurugenzi Mtendaji au kampuni inayodhibiti DigiByte blockchain. Watengenezaji na jamii ni watu wanaojitolea wasio na malipo kitu ambacho kinaondoa hatari ya kufilisika.

Haraka zaidi.

Miamala ya DigiByte inathibitishwa ndani ya sekunde 15 kwa makadrio, ambayo ni mara 40 haraka zaidi ya Bitcoin na mara 10 haraka zaidi ya Litecoin. SegWit inawezesha mpaka miamala/shughuli 1066 kwenye mnyororo kwa sekunde na kwa ada ndogo sana kabisa na kuifanya DigiByte sarafu bora ya malipo ya kila siku.

Salama wakati wote.

DigiByte imeundwa kwenye teknolojia mahili ya blockchain ya Bitcoin na kuweka vitu mahili kabisa juu yake kama DigiShield guard, MultiAlgo mining na Odocrypt algorithm. Pia Dandelion++ privacy protocol inasaidia kukuweka salama kwa kuficha IP na eneo ulilopo. Jifunze zaidi.

Inachimbwa.

DigiByte ni blockchain ambayo ni 100% Proof of Work (PoW) na inaweza kuchimbwa kwa algorithms 5 zinazoitwa Sha256, Scrypt, Skein, Qubit na Odocrypt. MultiAlgo mining inachangia madaraka (kutohodhiwa), usalama wa mtandao na kukupa uhuru wa kutumia vifaa tofauti kama ASIC, FPGA au GPU. Jifunze zaidi.

Vizio vinavyothibitiwa.

Ukilinganisha na Bitcoin milioni 21, DigiByte bilioni 21 (1000:1 kwa uwiano na BTC) zimetengenezwa tayari kwa ajili ya kupokelewa na watu wengi. DigiByte block rewards hupunguza 1% kila mwezi ya DigiByte zote badala ya kupunguza nusu ya block kila baada ya miaka 4. DigiBytes zote bilioni 21 zitakuwa zimechimbwa ifikapo mwaka 2035. Baada ya 2035 wachimbaji basi watategemea ada ya ununuzi peke yake. Jifunze zaidi.

Urahisi wa kuchagua kutoka kwenye mfumo wa DigiByte.

Kubadilishana yote na huduma zote zinazowezesha DigiByte zinapatika kwenye DigiByte Wiki.

Njia iliyorahisishwa
kuunda mali.

DigiAssets ni salama, safu ya juu yenye kuweza kupanuliwa ya blockchain ya DigiByte ambayo inawezesha utoaji madaraka ya mali/sarafu, smart contracts, digital identity na zaidi.

Jifunze kwa kutazama

Uwezo usio na kikomo.

DigiAssets zinaweza kutumiwa kuwakilisha usalama wa kitu chochote tunachopata katika ulimwengu. Kutoka kwenye mali inayoonekana kama vile mali isiyohamishika au magari, kupitia kwa uhaba wa vipande vya sanaa vya kidigitali. Hati zilizosainiwa kama vile shughuli na bili za matibabu zinaweza kulindwa pia.

Kukua kwa ujasiri.

DigiAssets kama mfumo wa ikolojia na jukwaa tayari lina vyama vyenye nia ya kupanga au kujenga majukwaa katika mali zisizohamishika, fedha, malipo, utambulisho, sehemu ya kuuzia, mbio, biashara, huduma za afya, mnyororo wa usambazaji, serikali na zaidi.

Teknolojia yenye uwezo.

DigiAssets inaleta huduma za kipekee za blockchain zilizoidhinishwa kupatikana ndani ya blockchain isiyo na ruhusa kama DigiByte. Hii inaruhusu DigiAssets kuwa salama zaidi, kupanuliwa na zisizoingiliwa na mtu yeyote kuliko jukwaa lingine lolote kwenye soko.

Anza sasa na DigiAssets.

Jifunze protakali.

Vumbua chanzo-wazi cha vigezo vya itifaki ya DigiAssets kwa ajili ya kutoa na kufanya miamala ya mali/sarafu za kidigitali kwa kutumia blockchain ya DigiByte. Itifaki ya DigiAssets kwenye GitHub, Mabadiliko na upanuzi wa DigiAssets Core.

Toa Mali/Sarafu ya kidigitali yako.

Sio mwana-programu? Kwa kweli sio shida! Mtu yeyote anaweza kutoa DigiAsset kwa urahisi kwa kutumia moja ya vifaa vinavyopatikana bila kuwa na ujuzi wa kiufundi juu ya itifaki. Huduma zinazoungwa mkono na DigiAssets.

Tunza / Fanya biashara.

Unajiuliza jinsi ya kutumia DigiAssets? Tembelea huduma zinazoungwa mkono na DigiAssets kununua, kuuza na kubadilisha DigiAssets.

Unahitaji msaada zaidi?

Je, unahitaji msaada zaidi kuhusu DigiAssets? Jisikie huru kujiunga na jukwaa la majadiliano la DigiByte kwenye GitHub na uulize maswali yako au ushiriki mawazo yako. DigiByte GitHub Majadiliano.

Uthibitisho bora.

Digi-ID ni itikadi ya usalama iliyojengwa juu ya teknolojia ya blockchain ya DigiByte kuwezesha watumiaji kuweka jitihada kidogo kuingia kwenye tovuti, programu na zaidi.

Jifunze kwa kutazama

Uthibitishaji rahisi.

Digi-ID inaondoa jina la mtumiaji, nenosiri na mahitaji ya uthibitisho wa 2fa. Kwa sababu Digi-ID hutumia kifunguo cha umma / kibinafsi cha faragha, hakuna manenosiri au majina ya watumiaji yaliyo hatarini. Njia hii sio tu inalinda watumiaji, inalinda pia huduma ambazo mtumiaji hutumia.

Usalama usio na usawa.

Digi-ID hahifadhi taarifa yoyote kuhusu watumiaji kwenye blockchain. Hii inaimarisha usalama na pia inazidisha ujasiri wa watumiaji wa mwisho kwamba taarifa zao hazifuatwi wala kuwa kwenye hatari kwa uzembe wa wengine. Hakuna hatua ya nje ya kutofaulu kwa mdadisi ili kulenga na kutumia jukwaa lako.

Rahisi na bure.

Digi-ID ni bure kabisa! Hakuna ada, huduma za usajili, au gharama za matengenezo. Lakini gharama ni sehemu yake ya pili ya ubora wa Digi-ID. Kipengele chake cha msingi ni kwamba, kulingana na kipaumbele cha usalama wa DigiByte, Digi-ID ni njia salama zaidi, lakini rahisi kupatikana kwa tovuti, programu na zaidi.

Inafanya kazi kama hivi.

Kizazi.

Tovuti, programu au bidhaa hutoa nambari ya kipekee ya Digi-ID QR na kuiwasilisha.

Ku-scan.

Mtumiaji huchambua nambari ya QR kutoka kwa programu yoyote inayoungwa mkono na Digi-ID.

Uthibitisho.

Mtumiaji huthibitisha ombi kwa kuingiza PIN yake au kwa ku-scan alama za vidole/uso wake.

Uthibitisho.

Digi-ID hutuma ombi lililosainiwa kwa njia ya maandishi na mtumiaji atafanikiwa kuingia.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara.

Ninaweza kupata wapi nyaraka zaidi?

Sehemu nzuri ya kuanzia ni Digi-ID.io. Ikiwa unataka kujua zaidi juu ya maelezo na faida za Digi-ID, unaweza kurejelea mwongozo wa mtumiaji, mwongozo wa muuzaji na mwongozo wa ujumuishaji. Ikiwa unatafuta vifaa vya habari, tafadhali pata karatasi ya utangulizi na nembo.

Maktaba za ushirikiano ziko wapi?

Kwa kuwa Digi-ID ni chanzo-wazi, unaweza kujifunza zaidi kwa kutembelea DigiByte Core Development. Ikiwa unahitaji msaada zaidi, tafadhali jiunge na jukwaa la majadiliano la DigiByte kwenye GitHub kuuliza maswali yako.

Je! Ninaweza kuingiza Digi-ID bila kujua programu?

Kama wewe sio mtengeneza programu, unaweza kutaka kutumia suluhisho jumuisho lililo tayari za kwa tovuti yako au bidhaa. Unaweza pia kutumia WordPress plugin kwa majukwaa ya WordPress.

Je! Kuna programu nyingine za utambulisho za Digi-ID?

Ndio! Digi-ID ni jukwaa linalokua haraka. Programu nyingi za uthibitisho na na pochi zinazoendana na Digi-ID zinapatikana katika sehemu ya Vipakuliwa.

Jamii inayopenda zaidi!

Makumi ya watu wa kujitolea kutoka ulimwenguni kote wamechangia DigiByte kwa njia mbalimbali kwa miaka kuifanya iwe kama ilivyo leo. Ni harakati ya kweli ya chini kwa chini. Tunakukaribisha kwa upendo ili ujiunge nasi!

Jifunze kwa kutazama

Watengenezaji wa programu za DigiByte.

Kila mtu anayefanya kazi kwenye DigiByte ni anajitolea bure bila malipo. Anza kuchangia maendeleo ya DGB leo au ujenge programu yako mwenyewe juu ya blockchain ya DigiByte.
Wakubwa wa DigiByte kwenye Majadiliano ya GitHub.
Itifaki ya DigiByte Core kwenye GitHub.

DigiByte Wiki.

The DigiByte Wiki ni makala ya mtandaoni iliyojengwa na jamii Kwa ajili ya jamii. Ina data muhimu na mpya kama vile Mfumo wa DigiByte na jinsi ya kuongoza. Mtu yeyote anaweza kuchangia kwenye Wiki kwa kuunda akaunti ya bure ya mtumiaji na kuanza kuongeza habari kwenye DigiByte Wiki.
Onyo Epuka kujitangaza kusio na haya na viungo vya mialiko.

Kiufundi Mfumo Utimilifu

Chagua programu yako.

Chagua programu kutuma, kukubali na kuhifadhi DigiBytes na DigiAssets zako au uthibitishe usalama kwa kutumia Digi-ID.
DigiByte Core ya sasa v8.22.1

Jifunze kwa kutazama

Itifaki & Mkoba
Yote Kwa Moja

DigiByte Core ina nakala kamili ya blockchain na inajenga uti wa mgongo wa mtandao. Mara nyingi hutumiwa na watengenezaji, masoko ya kubadilishana, na biashara nyingine, pamoja na wanachama wa jamii, kwa ajili ya kufanya mtandao kuwa wa kidecentrali kwa kuendesha node kamili. Pia inatumika kama mkoba wa programu.

DigiByte Core

  • Uthibitisho kamili
  • Usaidizi wa mtandao
  • Utulivu wa juu
  • Usaidizi wa SegWit

Inapatikana kwa Windows, macOS, Linux & Snapcraft (64 Bit)

Onyo la Mkoba
DigiByte Core kama mkoba inapaswa kutumiwa na watumiaji wa juu tu ambao wanajua jinsi ya kuweka mkoba wao salama. Ikiwa wewe si mtumiaji mwenye uzoefu, unaweza kutaka kutumia mkoba wa programu uliorahisishwa.

Hati za DigiByte na Miongozo.

Unatafuta nyaraka zaidi? Ikiwa unahitaji habari ya msingi ya kifungu au habari ya kiufundi kwa mchakato wa ujumuishaji. Unaweza kufikia miongozo yote muhimu hapa chini.

DigiByte Info Paper

Jifunze maelezo ya DigiByte blockchain kwa kutumia "info paper".

Info paper Pakua
DigiByte Integration Guide

Jumuisha blockchain ya DigiByte katika ubadilishanaji wako, pochi au huduma kwa urahisi.

Mwongozo wa ujumuishaji Pakua
DigiByte Media Sheet

Jifunze ukweli muhimu kuhusu blockchain ya DigiByte blockchain kwa kutumia karatasi ya media haraka.

Karatasi ya media Pakua
DigiByte Presentation

Tumia uwasilishaji wa mtandaoni unaofaa wa kutambulisha DigiByte kwa marafiki zako.

Uwasilishaji Anza
DigiByte Logos & Icons

Pata nembo na picha sahihi na za kisasa za DigiByte kwa ajili ya mradi wako.

Nembo na Picha Nenda GitHub
How to Guides

Endesha DigiByte yako mwenyewe kamili kwa kurejelea miongozo ya Wiki.

Jinsi ya kuongoza Nenda DigiByte Wiki